9 Mei 2019 - 14:30
 Hillary Clinton: serikali ya Trump si yakutekeleza makubaliano yeyote yaliopitishwa

Waziri wa mambo ya nje wa Zamani nchini Hillary Clinto ameikosoa serikali ya Marekani kwa kuendelea kuibana Iran na kusisitiza kuwa serikali ya sasa ya Marekani haiwezi kutekeleza makubalianoi yeyete yaliopitishwa kisheria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Hillary Clinton aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani katika utawala wa Baraka Obama, ambapo ametoa kauli yake kuhusu maamuzi ya Iran kusitisha kutekeleza baadhi ya mambo yaliokuwa katika mpango wa Nyuklia wa Iran, huku akionyesha kukata matumaini kufuatia kutokea kwa suala hili amesema: kwa hakika hali ya sasa ni ya hatari na inasikitisha sana, siwezi nikaifananisha na hali yeyote iliokuwa imeshatokea ambayo ni hatari zaidi ya halii.
Aidha ameendelea kubainisha hayo kwa kuashiria siasa ya kivita inayo endelezwa na Trump kwamba, kwa upande nahofia siasi shinikizo inayofanywa na serikali ya Marekani, ikiwemo kutoma Manuali za kivita katika ukanda wa mashariki ya kati, jambo ambalo linashadidsha hatari katika ukanda huo.
Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa nchi yetu inaserikali ambayo haikotayari kutekeleza makubaliano yeyete yalifikiwa kisheria, tija yake tunaona wairan nao wametangaza kusitisha kutekeleza baadhi ya mamnbo yaliokuwa ndani ya makubaliano ya mpango wa Nyuklia, mkwani sisi pia tulishakuwa tumeacha kutekeleza makubaliano ya mkataba huo.
mwisho/290